Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Chalamila: Polisi hawahusiki na utekaji

Chalamila Bombokoooooooo Chalamila: Polisi hawahusiki na utekaji

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema mkoa huo uko salama, hivyo wananchi wasiogope kutekeleza majukumu yao ya kila siku.

Ametoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya baadhi ya watu kushindwa kuendelea na majukumu yao kutokana na matukio ya ukatili ikiwemo mauaji, ulawiti na utekwaji yanayoendelea mkoani humo.

Akizungumza Dar es Salaam leo katika uzinduzi wa Kongamano la Matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia, Chalamila amegusia matukio ya utekaji na mauaji yaliyoripotiwa siku za karibuni jijini Dar es Salaam na kusema Jeshi la Polisi linasimamia na kufuatilia masuala hayo kwa karibu na tayari baadhi ya watuhumiwa wamekamatwa na taratibu za kisheria zinaendelea.

"Katika matukio haya polisi hawahusiki kwani wao wapo kwa ajili ya kulinda raia na watu wake na si vinginevyo, lakini pia jamii itambue polisi hawawezi kukulinda kila sehemu au kuingia ndani.

"Hata mimi nina walinzi lakini siwezi kuwa na mlinzi mpaka kitandani, hivyo usalama wa ndani unaanza na sisi wenyewe pia Jeshi la Polisi haliwezi kukuzuia kwenda kwa mganga ,"amesema.

Hata hivyo amesema mkoa ni mkubwa na kuna baadhi ya matukio kama udokozi na wizi haviwezi kukosekana, kwani hayo yote ni matokeo ya malezi ya baba na mama kwa mtoto, hivyo ni vyema kauli za Polisi kuteka zikakoma midomoni mwa watu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live