Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

CDF Mabeyo: Magufuli Aliniachia Dokezo, Nitakuja Ofisini Kwako

Video Archive
Fri, 26 Mar 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

CDF Mabeyo: Magufuli Aliniachia Dokezo, Nitakuja Ofisini Kwako March 26, 2021 by Global Publishers



Mkuu wa Majeshi nchini Tanzania (CDF), Venance Mabeyo ameomba kuonana na Rais Samia Suluhu Hassan ofisini kwake akibainisha kuwa kuna dokezo anataka kumpatia.

Mabeyo ameeleza hayo leo Ijumaa Machi 26, 2021 katika ibada ya mazishi ya Rais wa Awamu ya Tano Hayati John Magufuli wilayani Chato Mkoa wa Geita.

Alieleza hayo baada ya kuitwa kutoa salamu za pole kama ilivyokuwa kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria shughuli hiyo.

Huku akizungumza kuhusu kazi iliyofanywa na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) katika ujenzi wa ukuta wenye urefu wa kilomita 24 unaozunguka mgodi wa madini ya Tanzanite Mirerani wilayani Simanjiro Mkoa wa Manyara, aligusia suala hilo.

“Upendo wake kwa vyombo vya ulinzi na usalama aliuonesha kwa namna ambavyo alivishirikisha katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na maendeleo ya nchi yetu, alisema hatuwezi kuwa na vyombo imara bila kuwa na uchumi madhubuti.

“Mheshimiwa Rais (Samia) binafsi Hayati Magufuli alinidokeza, lakini ninaomba nisilitoe dokezo hilo nitakuomba nikuone ofisini….. Simanzi na masikitiko haya makubwa kwetu yanatokana na ukweli kwamba tangu aingie madarakani mwaka 2015 hayati Dkt. Magufuli alionesha kuviamini na kuvipenda vyombo vya ulinzi na usalama kwa dhati.

“Vyombo vyetu vimeaminiwa na kushirikishwa kwenye kuujenga uchumi wa nchi mfano mzuri ni kuulinda mgodi wa Tanzanite pamoja na miradi mbalimbali nchini ikiwemo ujenzi wa Ikulu Chamwino ambapo ujenzi wake uko katika hatua za kukamilika,” amesema Mabeyo.

Aidha, CDF Mabeyo amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ataitwa pia Amiri Jeshi Mkuu wa Tanzania na sio Amirat kama ambavyo ilipendekezwa…. “”Mh Rais, tunashukuru Baraza la Kiswahili la Taifa limerekebisha, utaendelea kuitwa Amiri Jeshi Mkuu na siyo Amirat kama ilivyokuwa inapendekezwa…”

Chanzo: globalpublishers.co.tz