Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

"CCM walimfanyia figisu Slaa" Magufuli atoa ya moyoni kumhusu Dr. Slaa (+video)

Video Archive
Sun, 25 Oct 2020 Chanzo: millardayo.com

Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, John Magufuli amefichua siri jinsi alivyomfahamu aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na Mbunge wa Jimbo la Karatu  Balozi Dkt. Willibroad  Slaa kwa jinsi alivyokuwa tofauti na wapinzani wengine.

Balozi Dkt. Slaa alihama CHADEMA wakati  vuguvugu la Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa Chama hicho kikiungana  na Vyama vilivyokuwa vikiunda UKAWA kumpitisha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kuwa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano .

Akizungumza Jimboni Karatu mkoani Arusha kwa ajili ya kuomba kura kwa wananchi, Magufuli amesema Balozi Dkt. Slaa alikuwa ni tofauti na wapinzani wengi  kwa jinsi  alivyokuwa mtu makini,mwenye kujenga hoja na alikuwa mwakilishi mzuri wa wananchi wa jimboni kwake.

“Wakati alipotaka kuja kuomba ubunge huku (karatu)aliomba nafasi hiyo kupitia Chama cha Mapinduzi kwasababu yeye alikuwa mwanaccm,Chama cha mapinduzi hapa karatu wakamfanyizia figisu hawakulirudisha jina lake ndipo akaamua kwenda mageuzi,”  JPM

“Balozi Dkt.Slaa baada ya kukaa upinzani na kuona ubabaishaji kwenye Chama hicho aliamua kujitoa katika Chama hicho,” JPM

Chanzo: millardayo.com