Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bulaya aitaka Serikali kulipa madeni ya vyombo vya habari

BULAYA Ml Bulaya aitaka Serikali kulipa madeni ya vyombo vya habari

Fri, 17 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge wa Viti maalumu, Ester Bulaya ameikumbusha Serikali kulipa madeni ya Vyombo vya Habari ili viwezi kujiendesha, kauli ambayo inakuja ikiwa wiki moja imepita tangu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko kuhimiza suala hilo.

Akiongea hii leo Mei 16, 2024 Bungeni Jijini Dodoma Bulaya amesema Serikali inadaiwa zaidi ya bilioni 18 na Vyombo mbalimbali vya Habari ambavyo vinategemea matangazo kutoka serikalini, huku akimuhoji Waziri wa Habari na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye kuhusu suala hilo.

Amesema, “wanapolipwa ndio wataanza kulipa mishahara, wataweza kujiendesha na hapo kuna baadhi ya vyombo vingine havijaorodheshwa katika madeni hayo, vyombo vingine binafsi zaidi ya bilioni saba ziko nje hawa watu watafanyaje kazi? Mhe. Nape sasa unadhani kwa madeni sugu hayo unadhani watajiendeshaje.”

Bulaya ameongeza kuwa, “Sisi waandishi wa habari kazi yetu kufanya kazi tu hatuna wa kututetea mpaka ifike leo humu ndani tuanze kuzungumza hii sio Sawa tunaomba hawa watu walipwe, mbona kuna taaluma nyingine hawakopwi, kuna taswira hapa imejengeka kama Wanahabari ni kama watu wamefeli sehemu fulani wamekuja kutafuta ajira, hii siyo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: