Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bulaya: Mkandarasi Bwawa la Nyerere anataka kuishtaki Serikali

BULAYA Ml Mbunge Ester Bulaya

Fri, 2 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mbunge Ester Bulaya amesema “Mkataba wa ujenzi wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere unaeleza mkandarasi akichelewa kukamilisha mradi anatakiwa kutozwa tozo, mradi ulitakiw akukamilika 2022 na taarifa zilizopi hautakamilika mwaka huu.

Amesema hayo Bungeni na kuhoji kwanini TANESCO hawajamtoza tozo Tsh. Bilioni 329 wakati Serikali ikichelewa kumlipa Mkandarasi inatozwa Tozo.

Aidha, amesema Mkandarasi alitakiwa kujenga miradi kwa ajili ya huduma za kijamii ya zaidi ya Tsh. Bilioni 200 lakini huduma hizo hazionekani, pia inadaiwa anajiandaa kufungua kesi Mahakamani dhidi ya Serikali akidai nyongeza.

“Kwa mujibu wa mkataba ambao mmeingia na mkandarasi, unataka mkandarasi akichelewa kukamilisha mradi anapaswa kutozwa tozo, sasa huu mradi ulipaswa kukamilika mwaka jana, unapaswa kukamilika mwaka huu ambapo imebaki siku 13, na taarifa zilizopo hautakamilika on time, utaenda mpaka mwakani Juni 7.

“Kwa nini mpaka sasa hivi TANESCO hajamtoza mkandarasi tozo? Kwa kutokamilisha mradi mwaka jana alitakiwa atozwe tsh bil 324, na Serikali imekuwa ikichelewa kuwalipa wakandarasi inatozwa tozo, kwa nini sisi tunapata kigugumuzi kuchukua hii tozo?

“Hii tunawafanya wakandarasi waone Tanzania ni kichwa cha mwendawazimu, wanaweza kufanya chochote wananchotaka. Tumeshindwa kusimamia mikataba yetu, nah ii haijaanza leo Tanesco, yalifanyika kwenye SIMBION, SONGAS na mengine, kuna tatizo gani? Lazima tujifunze pale tunapokosea.

“Kwa mujibu wa mkataba, Mkandarasi wa huyu alitakiwa ajenge miradi ya kijamii yenye thamani ya Tsh bil 200, lakini mpaka sasa hakuna mradi wowote wa kijamii na ni haki yetu na ‘alijikomiti’ kwamba atajenga.

“Ninaskia kwa mujibu wa mkataba, akijisikia anaweza kuongeza tu gharama ya mkataba, na tunataarifa kwamba ana mpango wa kufungua kesi, Waziri inabidi utuambie hili limekaaje. Wakati yeye hataki kutimimiza masharti ya mkataba lakini anataka kutupeleka mahakamani,” amesema Bulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: