Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Ole Sabaya Afikishwa Mahakamani - Video

Video Archive
Fri, 4 Jun 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Breaking: Ole Sabaya Afikishwa Mahakamani – Video June 4, 2021 by Global Publishers



Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha akiwa na wenzake watatu leo Ijumaa, Juni 4, 2021, ili kusomewa mashitaka yanayomkabili. Sabaya alisimamishwa kazi na Rais Samia Suluhu kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.



Sabaya amefikishwa mahakamani hapo chini ya ulinzi mkali wa polisi akiwa na walinzi wake sita na baada ya kushuka kwenye magari pamoja na wenzake walitakiwa kuchuchumaa kusubiri taratibu nyingine.

Baada ya muda mfupi walichukuliwa na kupelekwa katika chumba maalum wakisubiri kupelekwa mahakamani.



Kwa takribani wiki moja Sabaya alikuwa akihojiwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) kwa tuhuma mbalimbali jijini Dar es Salaam.



 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers)

Chanzo: globalpublishers.co.tz