Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Breaking: Ajali ya lori la mafuta na basi la Baraka yaua watu wanne - Video

Video Archive
Thu, 22 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa hii leo Agosti 22, 2024, kwenye ajali iliyohusisha lori la mafuta na basi la kampuni ya Super Baraka lililokuwa likitokea Dodoma kuelekea Dar es Salam, katika eneo la Vigwaza Chalinze mkoani Pwani.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani SACP Pius Lutumo amesema ajali hiyo imehusisha basi la Baraka lenye namba za usajiri T 277 DCN ambalo limegongana uso kwa uso na Lori la mafuta lenye namba za usajili RL 3520, katika eneo la Vigwaza, Kibaha, mkoani Pwani na kusababisha vifo vya watu hao watatu na majeruhi kadhaa.

Kamanda Lutumo marehemu hao ni wanawake watatu pamoja na mtoto mdogo ambaye umri wake haujafahamika na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa Kituo cha Afya cha Chalinze huku majeruhi wakikimbizwa Kituo cha Afya cha Mlandizi.

Akiongea kutoka eneo la tukio, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge amesema “Ajali imehusisha magari mawili, basi la abiria la Baraka lilikuwa likitoka Dodoma kwenda Dar es salaam na lori la mafuta lilikuwa likipeleka mafuta Rwanda limebeba mafuta ya petroli, taarifa ya awali imeonekana basi lilikuwa lina-overtake lakini lilipoona gari nyingine mbele likarudi upande wa pili na kugonga tenki la mafuta ubavuni”

“Tunasikitika kwamba matukio haya ya ajali yanaendelea kutokea na mara nyingi ni kutokana na uzembe , Dereva wa basi hajapatikana lakini tumepata madhara ya vifo Watu wanne ambao walikuwa abiria katika basi Watu wazima watatu na Mtoto mmoja wamefariki, tunaendelea na jitihada za kuhakikisha mafuta haya yanahifadhiwa vizuri ili tuondoe magari barabarani na kuondoa foleni barabarani, niombe Madereva wazingatie sheria za usalama barabarani.”

Kwa upande wake RPC wa Pwani, Pius Lutumo amesema taarifa zaidi kuhusu majina ya waliofariki na majeruhi yatatolewa baadaye “Tutoe wito kwa Madereva kuzingatia sheria za barabarani, eneo hili barabara imenyooka lakini Dereva wa basi kwa uzembe ameamua kutaka ku-overtake na kusababisha madhara haya”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live