Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Boti yazama Kigoma ikiwa na tani zaidi 120, mzigo ni wa Milioni 200 (+video)

Video Archive
Fri, 23 Apr 2021 Chanzo: millardayo.com

Boti ya mizigo iliyotambuliwa kwa jina la RUCHUGI 2 ambayo ilikuwa na zaidi ya tani 120 za bidhaa mbalimbali imezama katika bandari ndogo ya Kibirizi iliyopo Manispaa ya Kigoma Ujiji mkoani Kigoma na kusababisha hasara kubwa kwa wafanyabiashara waliokuwa wakisafirisha bidhaa hizo kwenda nchi ya Kidemocrasia ya Congo DRC.

Tukio hilo limetokea majira ya saa kumi na moja ya alfajiri ambapo boti hilo ambalo lililokuwa limepakia vyakula, Sariji na bidhaa zingine nyingi likiwa bandarini lilipigwa na wimbi kubwa na kugongwa kwenye chuma cha kivuko eneo la Bandari ya Kibirizi na kusababisha kuzama majini.

Hapa ni wakati shughuli za uokoaji wa bidhaa zikiendelea ambapo baadhi ya wasafirishaji wa bidhaa wananeleza hasara waliyoipata huku viongozi wa umoja wa wamiliki wa usafirishaji wa maboti mkoa akaiomba serikali kuchukua hatua ili kuondoa changamoto zilizopo.

Akizungumzia tukio hilo mkuu wa wilaya ya Kigoma Samson Anga amesema kutokana mabadiliko ya hali ya hewa kwa sasa Ziwa Tanganyika limejaa lakini pia kuongezeka kwa mawimbi ambapo amesema serikali inaharakisha ujenzi wa Bandari ili kuondoa changamoto zilizopo huku akitoa wito kwa wasafirishaji.

Chanzo: millardayo.com