Wakili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Hekima Mwasipu amesema Meya wa zamani wa Ubungo ambaye pia ni Kada wa Chama hicho Boniface Jacob, amekamatwa na Polisi akiwa maeneo ya Sinza na kupelekwa katika Kituo cha Polisi Oysterbay Jijini Dar es salaam leo September 18,2024.
Wakili Mwasipu amenukuliwa akisema; “Boni anatuhumiwa kwa kusambaza taarifa za uongo na muda sio mrefu wanakwenda kufanya upekuzi nyumbani kwake, muda huu tupo Oysterbay.”
Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime ametoa taarifa jioni hii akikiri Polisi kumshikilia Boniface Mkazi wa Mbezi kwa Msakuzi Jijini Dares Salaam kutokana na makosa ya kijinai anayotuhumiwa nayo “Wananchi wapuuze uongo unaosambazwa mitandaoni kuwa ametekwa.”