Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

‘Boni Yai’ asomewa mashtaka mawili, ombi la dhamana latolewa

Boni Yai Leo Kisutu ‘Boni Yai’ asomewa mashtaka mawili, ombi la dhamana latolewa

Thu, 19 Sep 2024 Chanzo: Mwananchi

Aliyekuwa meya wa Ubungo, Boniface Jacob, maarufu Boni Yai amesomewa mashtaka mawili ya kuchapisha taarifa za uwongo kwenye mtandao wake wa X (zamani Twitter), ambayo ameyakana.

Serikali imewasilisha maombi mawili, kwanza mahakama imuamuru aruhusu vifaa vyake vya kielektroniki pamoja na akaunti yake ya X ili mpelelezi aweze kuviingilia na kuvifanyia uchunguzi.

Pia, wameomba Mahakama izuie dhamana yake kwa muda. Sasa Mahakama inasikiliza maombi hayo na mawakili wa Serikali wanatoa hoja kufafanua msingi wa maombi hayo, kabla ya mawakili wa utetezi kuyajibu.

Boni Yai amepandishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jioni ya leo Alhamisi, Septemba 19, 2024.

Jopo la waendesha mashtaka mawakili wa Serikali wanaongozwa na Job Mrema pamoja na jopo la mawakili wa Jacob linaloongozwa na Peter Kibatala.

Chanzo: Mwananchi