Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biteko: SGR ni ushaidi tuna umeme wa kutosha

Treni SGR Biteko: SGR ni ushaidi tuna umeme wa kutosha

Thu, 12 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Ditto Biteko amesema safari za treni za Reli ya Kisasa (SGR) zinazotumia umeme kutoka Dar es Salaam hadi Dodoma ni ushahidi kuwa Tanzania ina umeme wa kutosha.

Dkt. Biteko ameyasema hayo baada ya kuwasili Jijini Dodoma akitokea Dar es Salaam kwa kutumia usafiri wa treni ya SGR kwa mara ya kwanza.

"Safari za treni ya umeme ya SGR ni ushahidi mwingine kuwa nchi ya Tanzania ina umeme wa kutosha, ni ushahidi mwingine kwamba nishati ya umeme ikipatikana ya uhakika inafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, viwanda mbalimbali vinajengwa na kongani za viwanda kuongezaka", amesema Dkt. Biteko

Katika kuhakikisha umeme unatosheleza Dkt. Biteko amesema Wizara ya Nishati kazi yake ni kuhakikisha umeme unakuwepo wa kutosha wakati wote na kuongeza kuwa wizara inasimamia ujenzi wa laini nyingine ya kuutoa umeme kutoka Chalinze kwenda Dodoma kwa laini kubwa zaidi na kutoa umeme kutoka Bwawa la kuzalisha umeme la Julius Nyerere kwenda Dodoma baadae Singida, arusha hadi Mwanza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live