Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Biden ampigia chapuo Harris Uraia Marekani

Biden Kamala.jpeg Biden ampigia chapuo Harris Uraia Marekani

Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Muda mchache kupita tangu, Rais wa Marekani, Joe Biden atangaze kutogombea tena nafasi hiyo katika muhula wa pili, amempigia chapuo makamu wake, Kamala Harris kupeperusha bendera ya chama cha Democratic katika nafasi hiyo.

Biden ameyasema hayo jana Jumapili Julai 21, 2024 kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twutter).

“Wanademocratic wenzangu, nimeamua kutokubali kuteuliwa na kugombea urais na kuhamishia nguvu zangu zote katika majukumu yangu kwa muda uliosalia wa muhula wangu.

“Uamuzi wangu wa mwaka 2020 ulikuwa kumchagua Kamala Harris kama Makamu wangu wa Rais. Na umekuwa uamuzi bora zaidi ambao nimefanya. Leo namuunga mkono Kamala kuwa mteule wa chama chetu mwaka huu, ni wakati wa kuungana kumshinda Trump,” amesema Biden.

Awali, Biden alipata shinikizo la kuondoka katika nafasi hiyo kutokana na hali yake ya kiafya kuzorota lakini pia kushindwa kufanya vizuri mdahalo na mpinzani wake Donald Trump.

Wiki iliyopita Biden aligundulika kuwa na Uviko-19 na kulazimika kutengwa hivyo kushindwa kuendelea na kampeni.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live