Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi miaka 85 adaiwa kuuawa na mfanyakazi wake wa ng'ombe - VIDEO

Video Archive
Tue, 23 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe limetolea ufafanuzi wa matukio Mawili ambayo yametokea mkoani Njombe.

Akizungumza na Waandishi wa habari Julai 22,2024 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Kamishna Msaidizi wa Polisi Mahamoud Hassan Banga amesema tukio la kwanza lilitokea tarehe Julai 20,2024 majira ya 19:00 hrs katika mtaa wa Idundilanga ambapo mama mwenye umri miaka 85 aitwaye Tulivane Mkongwa alikutwa ameuwawa na mtu ambaye anatiliwa mashaka aitwaye Petro Mhenga mfanyakazi wa Ng'ombe wa marehemu.

Amesema mtuhumiwa huyo alikimbia mara baada ya tukio kutokea lakini Jeshi la Polisi mkoa wa Njombe linawashikilia watu wanne ambao ni watoto wa marehemu kwa ajili ya upelelezi.

Katika tukio la pili, Kamanda Banga amesema tukio hilo lilitokea Julai 20,2024 majira ya saa 20:30hrs katika eneo la Uzunguni kata ya Ramadhani ambapo mfanyabiashara maarufu Njombe Godfrey Lwidiko Ndambo miaka 45, alivamiwa akiwa anatoka katika shughuli zake za biashara akiwa anaingia nyumbani kwake na kupigwa na kitu kizito kichwani na watu wasiofahamika na kutoweka na kiasi cha fedha kiasi cha shilingi milioni arobaini na saba.

Aidha Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhusiana na tukio hilo. Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana ili kupata taarifa na kuweza kuwatia mbaroni wahusika lakini pia linawashauri wananchi ambao wana kamera za nyumbani (CCTV) kuwasha wakati wote ili kupunguza matukio ya uhalifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live