Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bibi miaka 70 na mwanaye kizimbani kwa kusafirisha dawa za kulevya - VIDEO

Video Archive
Wed, 11 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bibi Felista Mwanri (70) na mtoto wake, Richard Mwanri (47) wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na tuhuma za kusafirisha zaidi ya tani moja ya dawa za kulevya aina ya bangi aina ya skanka.

Bibi Felista na mtoto wake wanashtakiwa pamoja na Athuman Mohamed maarufu kwa jila la Makame (58) mkazi wa Tanga, Juma Chappa (36) mkazi wa Kiwalani na Omary Mohamed (32) ambaye ni dereva anayeishi Buza, Dar es Salaam.

Katika hati ya mashtaka iliyosomwa mahakamani hapo na wakili wa Serikali Eric Davis mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Godfrey Mhini imedai washtakiwa wanatuhumiwa kwa shtaka moja la kusafirisha dawa za kulevya kinyume na sheria.

Imedaiwa, Agosti 28,2024 washtakiwa wakiwa eneo la Tairo Luguruni barabara ya Kwembe ndani ya Wilaya ya Ubungo ǰijini Dar es Salaam walikutwa wakisafirisha kilogramu 1815 za dawa za kulevya aina ya bangi.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na washtakiwa hawakuruhusiwa kujibu kitu chochote mahakamani hapo kwa kuwa kesi inayowakabili ni ya uhujumu uchumi. Wote wamerudishwa mahabusu.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Septemba 24,2024 kwa ajili ya kutajwa na kuangalia hatua ya upelelezi ilipofikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live