Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Bashe aitaka CCM isimamie misingi yake, Aja na hoja ya kukomesha mauaji na utekaji

Video Archive
Mon, 12 Mar 2018 Chanzo: bongo5.com

Mbunge wa Nzega Mjini kwa tiketi ya CCM, Mhe. Hussein Bashe amesema kuwa tayari ameshachukua hatua ya kuwasilisha hoja yake binafsi kwa Katibu wa Bunge na kudai kuwa ni wajibu wake kikatiba.

Hussein Bashe

Bashe amesema kuwa hoja hiyo haijatoka hewani ameshafanya utafiti wa kutosha kwa zaidi ya miezi mitano juu ya matukio ya utekaji, mauaji na watu kupotea yaliyotokea tangu mwaka 2010.

Akielezea hoja hiyo mbele ya waandishi wa Habari leo Alhamisi Machi 08, 2018, Mhe. Bashe amesema ili chama chake kiendelee kuimarika ni lazima kisimamie misingi yake.

Ili CCM iendelee kuimarika lazima isimamie misingi yake. Nakwenda bungeni na hoja hii kama mbunge wa CCM. Nimechukua hatua hii sababu ni kiapo changu kwa Chama Cha Mapinduzi. Siwezi kulalamika mitaani nitatumia nafasi yangu kuwasilisha jambo hili,” amesema Bashe.



Chanzo: bongo5.com