Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso atoa mwezi mmoja maji yapatikane Simanjiro

Awesooo At 16.jpeg Aweso atoa mwezi mmoja maji yapatikane Simanjiro

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya Wananchi zaidi ya 200 kuaandamana na kufunga barabara kwa zaidi ya saa sita kwa madai ya ukosefu wa maji katika kijiji cha Losintai katika kata ya Oljoro namba tano Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Waziri wa Maji Jumaa Aweso ameingilia kati jambo hilo na kuagiza kuwa mpango huo unatakiwa kukamilika ndani ya mwezi mmoja Wananchi waanze kupata maji.

Meneja wa Wakala wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini RUWASA Mkoa wa Manyara amesema mradi wa upatikani wa maji ulikuwa kwenye mpango na ulikuwa ushaanza kutekelezwa na leo Waziri wa Maji Juma Aweso amempigia simu na ametaka maji yapatikane September 30, 2024

“Mkuu wa Wilaya mpango uliopo katika kijiji cha Lesinyai unafahamika, baada ya tukio la jana sisi tuna mifumo yetu ya kutoa taarifa za miradi, Viongozi wangu akiwemo Waziri wa Maji alinipigia na akaridhia mpango huu ukamilike September Watu wapate maji,” amesema Mhandisi Wolter Kirita Meneja RUWASA.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Simanjiro Fack Lulandala amekutana na Wananchi kwenye mkutano wa hadhaea na kuongea nao mambo mbalimbali na amewaagiza Polisi kutokutumia bomu hata moja kwa Wananchi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live