Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso akamilisha kazi ya wiki kwa siku 1 Buhongwa, kazi yakamilika usiku

Video Archive
Mon, 9 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso amehakikisha Kazi iliotakiwa kufanyika ndani ya wiki moja ya ukamilishaji wa Mradi wa Maji wa Buhongwa jijini Mwanza ilitokiwa kukamilishwa mpaka ijumaa inafanyika ndani ya siku moja kwa kuamua kuweka kambi na mafundi site mpaka saa sita usiku.

Mradi wa dharula Buhongwa umekamilika usiku na Maji rasmi yamefika hapa Buhongwa Centre na kazi itakayofuata ni kuunganisha kwa wananchi.

Awali Waziri Aweso ameshuhidia maunganisho ya bomba ya mwisho ya mradi wa Sahwa Buhongwa ambao unalenga kutatua changamoto katika maeneo ya Sahwa, Lwanhima na Buhongwa.

Mara baada ya bomba la mwisho kuunganishwa saa 4.15 usiku alielekea katika kituo cha kusukuma maji Sahwa ili kuwasha pump ya maji kwa lengo la kusafisha bomba hilo.

Usiku huo huo Waziri Aweso amewakabidhi wenyeviti wa serikali za mitaa za Sahwa chini na Semba mabomba kwa ajili ya kusogeza maji katika maeneo yao.

Mradi huu una gharama ya Tshs. Milioni 864.816. Mradi huu utanufaisha wakazi wa mitaa ya Sahwa ya chini, Sahwa ya juu, Buhongwa mashariki, Buhongwa magharibi, Buhongwa centre na Maliza.

Jumla ya vituo nane vya kuchota maji vitajengwa katika maeneo hayo na kunufaisha wananchi katika mitaa husika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live