Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aweso Amkaanga Meneja DAWASA Kigamboni "Kwa Nini Wananchi wanakosa Maji?" - Video

Video Archive
Thu, 4 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Maji Mhe Jumaa Aweso leo tar. 04 Julai 2024 amefika Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar Es Salaam kutembelea na kukagua Mradi Mkubwa wa Maji katika Miundombinu ya Tenki la Maji lita mil.15. Waziri Aweso anaendelea na ziara ya kikazi mkoa wa Dar Es Salaam.

Waziri Aweso amemtaka Meneja wa DAWASA Kigamboni kufanya kazi kwa bidii na kuboresha utendaji kazi wake na kuahidi kufanya mabadiliko makubwa wilaya ya Kigamboni kwani halizishwi na utendaji kazi wa eneo hilo.

Katika hatua nyingine Mhe Aweso amekutana na Watumishi wa mkoa wa DAWASA - Kigamboni ambapo amewasisitiza watumishi kufanya kazi kwa bidii na kudumisha umoja ili kuleta maendeleo katika mkoa wa Dar es Salaam.

Waziri Aweso pia ameelekeza uongozi wa DAWASA kuboresha huduma ya maji Kigamboni ili kila mwananchi anufaike na huduma ya Maji.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live