Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka bubu

Kijana Elias Ahukumiwa Jela Kwa Kumbaba Bibi (81) Atupwa jela miaka 30 kwa kumbaka bubu

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Babati mkoani Manyara imemtia hatiani kijana Ramadhani Iddi Kipusa (19) kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kwa makosa mawili ya kumbaka na kumlawiti binti mlemavu (bubu) mwenye umri wa miaka 19.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu wa Mahakama ya Wilaya ya Babati, Martin Masao amesema mahakama hiyo imeridhika na ushahidi wa mashahidi 19 uliotolewa kuwa mtuhumiwa ametenda makosa mawili ya kubaka na kulawiti, tukio lililotokea Februari 6, 2024 katika eneo la Magugu wilayani Babati.

Imedaiwa mahakamani hapo kuwa mtuhumiwa siku ya tukio, majira ya asubuhi aliingia ndani nyumbani kwa binti huyo wakati mama yake alipotoka kufuata mahitaji dukani na wakati anarudi ndipo alipokutana na sauti ya kulalama ya binti yake akiwa kitandani akiwa hana nguo za ndani huku akimuonesha mama yake kwa ishara kuwa nyuma ya mlango yupo mtu amejificha ambaye ni mtuhumiwa huku suruali yake ikiwa chini ya magoti.

Hakimu Masao amesema mahakama imeridhika na ushahidi na kumtia hatiani mtuhumiwa kwa kosa la kubaka ambayo kinyume cha kifungu cha 130 (1) ya sheria ya makosa ya jinai na kifungu kidogo cha 2 (a) cha sheria hiyo ikisomwa pamoja na kifungu 131(1) ambacho kinatoa adhabu, na kosa la pili la kulawiti kinyume cha kifungu cha sheria namba 154 (1)(a) cha sheria ya kanuni za adhabu sura namba 6.

Kwa makosa hayo, Kijana Ramadan atatumikia kifungi cha miaka 30 jela kwa kila kosa ambapo atatumikia kwa wakati mmoja na atatakiwa kumlipa muathirika wa tukio hilo fidia ya shilingi laki 5 kwa kila kosa baada ya kutoka gerezani.

Chema Maswi, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali Mkoa wa Manyara amesema upande wa jamhuri umeridhishwa na hukumu hiyo na kwamba itakuwa fundisho kwa watu wengine wenye tabia za kufanya matukio ya ukatili wa kijinsia hasa kwa makundi ya watu wenye ulemavu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live