Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, CHADEMA, Tundu Lissu katika muendelezo wa kampeni zake Jijini DSM ambapo zimefanyika katika viwanja vya Liwiti Tabata amesema Nchi inahitaji maridhiano ya kitaifa.
Amesema katika siku 100 za kwanza baada ya kupata ushindi katika uchaguzi utakaofanyika Oktoba 28, ataunda tume kwa ajili ya upatanishi na ukweli ili kuvumbua mabaya yanayofanyika katika nchi.
‘‘Nikiingia madarakani baada ya uchaguzi mkuu mwaka huu katika siku 100 za kwanza nitaunda Tume ya upatanishi na ukweli ili tufahamu mambo yote haya mabaya ambayo yamefanyika katika nchi yetu, tuwafahamu walioyatenda, tufahamu kwanini waliyatenda, nani aliyewatuma halafu tuwaambie tubuni dhambi zenu’’ Lissu