Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Askofu Bendera achafukwa utekaji watoto: Kwa lazima uue mtoto ili upandishwe cheo? - Video

Video Archive
Mon, 29 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Askofu Mkuu wa Makanisa ya Ufunuo, Paul Bendera amekemea vitendo vya baadhi ya watu ambao wamekuwa wakiiba watoto na kuwafanyia ukatiri ikiwemo mauaji na kuwanyofoa baadhi ya viungo vyao ili wapate mafanikio huku chanzo kikidhaniwa kuwa ni imani za kishirikina.

Bendera amesema hayo jana Jumapili kwenye ibada ya misa huku akisema kuwa watumishi au mtu yeyote ambaye anadhani anaweza kufanikiwa kwa kuua mtoto wa mwenzake anafanya makosa na kumuudhi Mungu, badala yake wanapaswa waamini kuwa kila jambo jema linatoka kwa Mungu hivyo wamtegemee Mungu pekee ndiye anaweza kukufanya vyovyote unavyotaka wala si ramli chonganoshi za waganga.

Kauli hiyo ya Bishop Bendera inakuja huku kukiwa na wimbi la utekaji watoto jambo ambalo hata Rais Samia Suluhu Hassan amelikemea na kuagiza jeshi la polisi na vyombo vingine vya sheria kufanya uchunguzi ili kuwabaini wanaofanya vitendo hivyo ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live