Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Asilimia 53.4 ya Watanzania wamechanja - Ummy Mwalimu

Waziri Ummy3c3c3ad0b068 780x470 Asilimia 53.4 ya Watanzania wamechanja - Ummy Mwalimu

Fri, 12 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema asilimia 53.4 ya Watanzania wamechanjwa chanjo ya UVIKO-19.

Waziri Ummy ameyasema hayo leo Mei 12, 2023 Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akiwasilisha bajeti ya wizara yake.

"Wizara imeratibu upatikanaji wa chanjo dhidi ya UVIKO-19 kupitia mpango wa kidunia kuhakikisha nchi zinapata chanjo ya UVIKO-19 (COVAX facility) na misaada kutoka nchi rafiki. Hadi kufikia mwezi Machi, 2023 jumla ya dozi 46,848,520 zilikuwa zimepokelewa na kusambazwa ambapo dozi 39,187,358 (sawa na asilimia 84) zimetumika hadi sasa.

Wizara inaendelea kuratibu utoaji wa chanjo ya UVIKO -19 kupitia vituo vya kutolea huduma za Afya vya umma na binafsi, huduma za mkoba na kampeni. Jumla ya vituo vya kutolea huduma 7,200 vinatoa huduma ya chanjo ya UVIKO-19 hapa nchini. Hadi kufikia mwezi Machi 2023 jumla ya watu 32,735,546 ambao ni sawa na asilimia 53.4 ya watanzania wote walikuwa wamekamilisha chanjo dhidi ya ugonjwa huu.

Chanjo hii imeweza kujenga kinga kwenye jamii hivyo kupunguza hatari ya kuugua ugonjwa huu na hata waliougua kutopata madhara makubwa.

Katika kipindi cha Julai 2022 hadi Machi 2023, kumekuwa na wastani wa visa 302 kwa mwezi bila kifo ikilinganishwa na kipindi kama hiki 2021/22 ambapo kulikuwa na wastani wa visa 1,557 na vifo 43 kwa mwezi." alisema Waziri Ummy.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live