Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuwekea sumu mwenzake ahukumiwa kunyongwa hadi kufa - VIDEO

Video Archive
Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la polisi Mkoa Morogoro limefanikiwa kupata mafanikio katika kesi mbalimbali na kupata vifungo kwa washtakiwa ambao walikamatwa na kufikishwa katika Mahakama mbalimbali za mkoa wa Morogoro

Akitoa taarifa yake kwa waandishi wa Habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama amesema kuwa jumla ya washtakiwa 73 walipatikana na hatia na kufungwa vifungo au kutozwa faini katika Mahakama za kawaida

Kamanda ametaja fanikio Moja wapo ni kesi ya Juma Salim (34) Mkulima na mkazi wa miembeni Wilaya ya Mvomero amehukumiwa na Mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Morogoro kunyongwa Hadi kufa Baada ya kupatikana na hatia ya mauaji ya Hussein Juma ambayo yaliyokea Dec 3 2022 Kwa kumuwekea Sumu kisha kumfukio kwenye shimo la choo

Chanzo: www.tanzaniaweb.live