Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Aliyemuua mkewe kwa kumchoma moto agoma kupimwa akili Mirembe

MAUAJI MKEWE Aliyemuua mkewe kwa kumchoma moto agoma kupimwa akili Mirembe

Thu, 25 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mfanyabiashara Khamis Luwonga (38) anayetuhumiwa kumuua mkewe Naomi Marijani na kumchoma moto kwa kutumia magunia mawili ya mkaa amekataa kwenda kupimwa akili katika Hospitali ya Mirembe akidai kuwa ana akili timamu, haumwi na hajisikii tofauti kwenye mwili wake.

Hata hivyo, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam imetoa amri kwamba ni lazima aende kupimwa ili ilijidhishe kwamba siku ya tukio alikuwa ana hali gani.

Luwonga amedai hayo leo mbele ya Jaji Elizabeth Mkwizu wa Mahakama hiyo , wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya ombi lililotolewa na Wakili wa mshtakiwa, Mohamed Majaliwa la kutaka mteja wake akapimwe akili Mirembe.

Mshtakiwa huyo, alifikia hatua hiyo ya kukataa kwenda kupimwa akili, baada ya upande wa mashtaka kusoma ombi la Majaliwa mbele ya mahakama ndipo akanyoosha mkono wake nakutaka kuzungumza.

Jaji Mkwizu alimpatia nafasi hiyo,  Luwonga amedai kuwa yeye hayuko tayari kwenda Mirembe kupimwa akili, kwa sababu ana akili timamu, haumwi wala hajisikii tofauti katika mwili wake.

"Mimi siko tayari kwenda Mirembe nina akili zangu timamu, labda kama nitalazimishwa nitaenda, lakini siyo kwa hiari yangu mwenyewe kwa sababu siumwi wala sijisikii tofauti yoyote," amedai Luwonga.

Baada ya mshtakiwa kudai hayo, Jaji Mkwizu alimueleza kuwa hata kama wakili wake asingeomba yeye kwenda kupimwa, lakini mahakama yenyewe lazima ingejilidhisha kutokana na tukio lililotokea, lazima aende kufanyiwa uchunguzi siku ya tukio alikuwa kwenye hali gani.

Jaji Mkwizu alimueleza kuwa mtu yeyote mwenyewe hawezi kuijua kama anautofauti au hana utofauti ndiyo maana anatakiwa akapimwe.

Hata hivyo, Jaji Mkwizu alitoa amri ya mshtakiwa kwenda kupimwa Mirembe. Kwa upande wa mshtakiwa yeye alikuwa amesimamia msimamo wake kwamba yupo timamu na kama kesi iendelee kusikilizwa.

Awali, mshtakiwa baada ya kumaliza kusomewa maelezo ya mashihidi 28 na vielelezo 14 na upande wa mashitaka, alidai kuwa yeye hakuua kwa makusudi na kwamba  hata anyongwe hadi kufa, ataangamia kimwili lakini sio kiroho.

Pia, alidai kuwa haogopi kunyongwa wala haogopi adhabu yoyote ile, lakini nataka kama akinyongwa basi ni anyongwe kwa haki kwamba aliuwa bila kukusudia, kwa sababu ni ajali tu ilitokea.

Katika kesi hiyo ya muaji namba nne ya mwaka 2019, mshitakiwa Luwonga ambaye ni Mkazi wa Kigamboni, Dar es Salaam anadaiwa Mei 15, 2019 akiwa Gezaulole eneo la Kigamboni alimuua Naomi Marijani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live