Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Alichokisema Majaliwa msibani kwa AG Kilangi

70387 Pic+majaliwa

Wed, 7 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mwanza. Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa amemsihi Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa nchi hiyo, Profesa Adelardus Kilangi kuwa mtulivu wakati wa kipindi kigumu cha kuondokewa na mkewe Natalia.

Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Jumatano Agosti 7, 2019 wakati akiongoza ujumbe wa Serikali ya Tanzania katika ibada ya mazishi ya Natalia katika kata ya Luchelele wilayani Nyamagama jijini Mwanza.

Majaliwa amesema Serikali ipo na yeye (Kilanga) katika kipindi hiki kigumu.

"Mheshimiwa Rais (John Magufuli) amepokea msiba huu kwa huzuni kubwa, ameniagiza ni mwakilishe alitamani kuwapo lakini kulingana na majukumu aliyonayo ya ugeni wa SADC ameshindwa kufika," amesema

"Professa Kilangi anafanya kazi vizuri sana, kwa weledi na upole lakini alikuwa akipata utulivu kutokana na uwapo wa mama Natalia.”

Majaliwa amesema, "Jambo hili ni zito sana huwezi kulipokea kwa haraka hata nasi limetugusa sana, wajibu wetu sisi waombolezaji ni kumuombea marehemu  lakini pia kumuombea Professa Kilangi apate utulivu.'

Pia Soma

Amesema jambo hilo ni uamuzi wa Mungu mwenyewe, "tunakusihi uwe mtulivu na watoto wako, sote tupo nawe.”

Chanzo: mwananchi.co.tz