Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua wanne wakiwemo wanafunzi Manyara

IMG 2ajaliA0001 Ajali yaua wanne wakiwemo wanafunzi Manyara

Sat, 31 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamepoteza maisha yao wakiwemo Wanafunzi watatu na Dereva mmoja katika ajali iliyohusisha Coaster na gari la mizigo aina ya Scania.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo August 31,2024 katika eneo la Gajal Babati Mkoani Manyara ambapo Coaster ilikuwa imebeba Wanafunzi kutoka Hanang kuelekea Mkoani Arusha na baada ya Kufika eneo hilo iligongana uso kwa uso na Scania.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Manyara Ahmed Makarani amesema chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa Dereva wa lori kushindwa kuwa makini barabarani na kuigonga Coaster hiyo iliyokuwa imebeba Wanafunzi 33 wa Shule ya Sekondari Endasaki waliokuwa wakielekea Mkoani Arusha kwa ajili ya likizo baada ya kufunga Shule.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live