Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua wanne Tanga

Video Archive
Mon, 17 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu wanne wamekufa papo hapo na wengine wanne kujeruhiwa kufuatia ajali ya lori la mizigo kugonga basi dogo la abiria “Coaster” katika eneo la Tanganyika, wilayani Muheza mkoani Tanga.

Lori hilo lenye namba za usajili T 925 CAU liliiparamia Coaster aina ya Nissan Civilian T 228 DPD iliyokuwa imeharibika barabarani wakati likitoka Muheza kuelekea Tanga Mjini.

Kamanda wa Polisi ACP Maket Msangi amesema ajali hiyo imetokea June 15, 2024 majira ya Saa 3 usiku ambapo Jeshi linaendelea kumsaka dereva wa lori la mizigo aliyetambulika kwa jina la Alvis Livingston pamoja na dereva wa Coaster ambaye jina lake halijafahamika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live