Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali yaua Watawa watatu (+Video)

Video Archive
Fri, 12 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Abate wa Abasia ya Ndanda Christian Temu OSB, ametoa taarifa ya kuthibitisha vifo vya Watawa watatu wa Shirika la Mtakatifu Benedikto Ndanda Mkoani Mtwara, waliofariki kutokana na ajali ya gari katika Kijiji cha Mtua Longa Halmashauri ya Mtama Mkoani Lindi mapema leo July 12,2024 baada ya gari dogo walilokuwa wakisafiria lenye namba za usajiri T 139 DZZ kuacha njia na kuangukia kwenye Korongo.

Watawa hao walikuwa wanaelelea Dar es salaam wakitokea Ndanda ambako jana July 11,2024 kulifanyika sherehe za nadhiri za muda na za daima.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo waliofariki ni Padre. Comellius Mdoe OSB, Padre Pius Boa OSB na Bruda Bakanja Mkenda OSB ambapo Dereva aliyekuwa anaendesha gari hiyo amepata majeraha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kusema chanzo cha ajali ni gari kupiga shimo na kupoteza mwelekeo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live