Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya basi yaua 11, yajeruhi 44 Mbeya - VIDEO

Video Archive
Fri, 6 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu 11 wamepoteza maisha na wengine 44 wamejeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya A-N Coach kupata ajali katika eneo la Luanjilo Wilaya ya Mbeya Vijijini.

Ajali hiyo imetokea alfajiri ya leo Ijumaa, Septemba 6, 2024 baada ya basi hilo lililokuwa likitoka Mbeya kwenda Tabora kupinduka wakati likilikwepa lori, kisha kutumbukia mtaroni.

Mganga wa Mkuu wa Hosptali ya Wilaya ya Chunya, Dk Darson Andrew amethibitisha kupokea idadi ya hiyo na vifo huku akieleza kati ya majeruhi 44 wanne wana hali mbaya na watapewa rufaa kupelekwa Hosptali ya Rufaa Kanda ya Mbeya.

Juhudi za kumtafuta Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya ili azungumzie ajali hiyo zinaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live