Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ajali ya basi la Zube yaua watatu Singida

Video Archive
Mon, 22 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Watu watatu wameripotiwa kufariki na wengine nane kujeruhiwa baada ya basi la Kampuni ya Zube lenye namba za usajili T-695-DDJ likitokea Mkoani Mwanza kwenda Dar es Salaam kugongana na lori katika kijiji cha Njirii Wilayani Manyoni Mkoani Singida.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, inaelezwa kuwa lori aina ya Eicher lenye namba T-908-DVX iliyokuwa imebeba chupa za soda likitokea Itigi kwenda Singida, liligongana uso kwa uso na kusababisha vifo hivyo.

Miongoni mwa watu waliofariki ni dereva wa basi na wa gari hiyo.

Juhudi za kumtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Singida SACP Amon Kakwale ili kuzungumzia tukio hilo zinaendelea.

Ajali hiyo imetokea ikiwa ni takribani siku 11 tu tangu ajali nyingine ya Basi la Zube Trans lililokuwa likitokea Dar kwenda Mwanza kupata ajali katika eneo la kijiji hicho hicho cha Njirii na kujeruhi watu 28 huku watu 52 wakinusurika kufa baada ya basi hilo kugongana na lori lililokuwa likitokea Rwanda kwenda Dar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live