Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ahukumiwa miaka 3 kwa kutoa hongo ya laki 1

Video Archive
Tue, 7 Jul 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza, imemhukumu kifungo cha miaka mitatu au kulipa faini ya Shilingi laki nane raia mmoja wa China, anayekabiliwa na shtaka la kutoa rushwa kiasi cha shilingi laki moja ili arejeshewe mashine yake ya kuchezeshea mchezo wa bahati nasibu.

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Theopista Sivoke, baada ya raia huyo wa China anayefahamika kwa jina la Sheng Bing Lin, kukiri kutenda kosa hilo kwa kumshawishi Afisa Mtendaji ampe rushwa ili amrudishie mashine yake.

Awali akitoa taarifa ya kukamatwa kwa raia huyo wa kigeni Naibu Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mwanza Daudi Ndyamukama, amesema kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo kinyume na kifungu cha sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa namba 11 ya mwaka 2007.

Ambapo mara baada ya hukumu hiyo kutolewa, Sheng Bing Lin alifanikiwa kulipa faini hiyo na kubaki huru.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live