Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la Waziri Nchemba kama huna kitambulisho cha utaifa (+Video)

833 Mbaa 640x400 TZW

Sat, 30 Dec 2017 Chanzo: millardayo.com

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dr. Mwigulu Nchemba akiwa kwenye ziara ya kikakzi mkoani Ruvuma ameagiza kila mtanzania kujiandikisha kupata kitambulisho cha taifa kwakuwa sio jambo la hiari bali ni lazima kwa kila Tanzania aliyeko ndani ya mipaka ya nchi kutambuliwa.

“Hili zoezi la vitambulisho vya utaifa ni lalazima kwa kila mtanzania aliye nchini, ni kosa kubwa kama wewe ni raia ukaamua kukaidi ikiwa Rais wetu Magufuli ameamua kutoa vitambulisho hivyo bure bila malipo yoyote”–Dr Nchemba

“Hili ni jambo la Nchi na ni kubwa hivyo tusililinganishe na jambo lingine lolote, baada ya mchakato huu kuisha tukamkuta mtu hana kitambulisho maelezo yake yatakuwa ni magumu kueleweka kama kweli yeye ni mtanzania halali” –Dr Nchemba

“Kwenye kupiga rungu siangalii mtu usoni” -Juliana Shonza

Chanzo: millardayo.com