Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la Waziri Dr. Mwigulu Nchemba kwa madereva wanaondesha magari kwa speek kali

5838 Mwigulu TZW

Thu, 5 Apr 2018 Chanzo: mtanzania.co.tz

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza polisi kumkamata dereva yeyote atakayeonekana anaendesha gari kwa mwendo kasi na asiachiwe hadi atakapofikishwa mahakamani.

Amesema mahakama ikijiridhisha kuwa ni kawaida ya dereva huyo kuendesha kwa mwendo basi dereva huyo anyang’anywe leseni.

“Pia nasisitiza kila basi la abiria liwe na madereva wawili ili mmoja akikamatwa mwingine aendelee na safari,” amesema Mwigulu.

Hatua hiyo imetokana na mwongozo ulioombwa na Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga alioomba kutokana na ajali iliyotokea jana ilisababishwa na shimo barabarani ambapo alitaka Wakala wa Barabara (Tanroads) watozwe faini kwani wamekuwa wakitoza watu faini bila sababu.

Akijibu hoja hiyo, Mwigulu amesema ajali ile haikusababishwa na shimo isipokuwa mwendo kasi.

Chanzo: mtanzania.co.tz