Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL Halina Thamani Sababu ya Madeni - Video

Video Archive
Thu, 22 Apr 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

ATCL Linaokana Kama Halina Thamani Sababu ya Madeni – Video April 22, 2021 by Global Publishers



Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaangalia namna ya kulilea Shirika la Ndege nchini (ATCL) kimkakati ili lijiendeshe kwa ufanisi.

Amesema hilo litafanyika kwa kuangalia uwezekano wa kutoa nafuu wa madeni na baadhi ya kodi na tozo kama inavyofanyika katika nchi nyingine ili liweze kukua na kuweka hesabu zake sawa.

Kiongozi mkuu huyo wa nchi ameeleza hayo leo Alhamisi Aprili 22, 2021 wakati akilihutubia Bunge mjini Dodoma.

“Shirika letu sasa hivi linasomeka kwamba ni shirika la deficit, halina thamani lakini ni kwa sababu ya kurithi madeni makubwa ya nyuma, hivyo kama Serikali tunakwenda kulitua mzigo wa madeni makubwa.”

“Pia tutalipa unafuu wa kodi na tozo ili liweze kukua, sote tunafahamu kuwa biashara ya ndege ni ngumu, tutajitahidi kusoma mwenendo wa biashara hii ulimwenguni na kuepuka mambo yote yasiyo na tija kwa Taifa letu,” amesema.

Amesema Serikali haitakubali kuona shirika linaendelea kupata hasara baada ya uwekezaji mkubwa na kwamba uwekezaji pia utafanyika kupata rasilimali watu wenye uwezo na weledi wa kuendesha shirika kibiashara.

Chanzo: globalpublishers.co.tz